Mkhitaryan
Man
Utd
MANCHESTER United imeingia kwenye rada za Juventus na Arsenal
za kumuwania kiungo wa Borussia Dortmund, Henrikh Mkhitaryan, ambaye amegoma
kusaini mkataba mpya na klabu yake hiyo.
CHANZO: Daily Mail
Azpilicueta
Barcelona
BARCELONA imatajwa kumuwania beki wa pembeni wa Chelsea,
Cesar Azpiliceuta ikiwa watamkosa Hector Bellerin wa Arsenal ambao nao pia
wanataka kumpa mkataba mpya wa kumbakiza Emirates.
CHANZO: Daily Telegraph
Morata
Man
Utd
STRAIKA Alvaro Morata wa Juventus anaona ni afadhali
ajiunge na Manchester United kuliko Chelsea. Kocha mpya wa kikosi cha United,
Jose Mourinho amekuwa akitajwa kuwa moja kati ya wachezaji walio kwenye mkakati
wa kuwasajili ni Morata.
CHANZO: Onda Cero
Denis
Suarez
Barca
MABINGWA wa La Liga, Barcelona imefanya makubaliano na
straika wa Villarreal, Denis Suarez kwenye ishu ya mshahara. Staa huyo atakuwa
mchezaji wa kwanza kusainiwa kwenye kikosi hicho.
CHANZO: Sport
Nani
Man
United
KOCHA mpya wa Man United, Jose Mourinho anataka kumrudisha
winga wa zamani wa kikosi hicho, Mreno mwenzake, Nani anayekipiga Fenerbahce.
CHANZO: DHA, via Talksport
Batshuayi
Chelsea
CHELSEA ipo tayari kuweka fedha mezani pauni milioni 31 ili
iweze kumnasa straika wa Marseille, Michy Batshuayi. Nyota huyo mwenye miaka 22
pia anawaniwa vikali na klabu za West Ham na Tottenham zote zinashiriki
Premisership.
CHANZO: Daily Mirror
Vardy
Arsenal
MSHAMBULIAJI wa Leicester City, Jamie Vardy ambaye
anawindwa na Arsenal kwa udi na umvumba, amejipanga kuipiga chini ofa ya
kujiunga na The Gunners. Imeripotiwa kuwa Arsenal wapo tayari kutoa pauni
milioni 20 na mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki ili impate lakini nyota huyo
ameambiwa na wenzake abaki King Power.
CHANZO: Evening Standard
Darmian
Juventus
MAN United imeripotiwa kutaka kumtumia beki wake Matteo
Darmian kama chambo ya kumpata kiungo wa Juventus, Paul Pogba. Imeripotiwa kuwa
Darmian alikuwa akichunguzwa na Juve sasa Kocha Jose Mourinho anataka kutumia
nafasi hiyo ili kufanikisha upatikanaji wa Pogba pamoja na kuongezea fedha
kidogo.
CHANZO: Evening Standard
Post a Comment