Sasa unaweza kuwapigia kura wachezaji sita waliobakia kwenye hatua ya fainali. Fuata hatua zifuatazo wakati wa kupiga kura kwa mchezaji husika;
Anza kwa kuandika jina lake, kisha mbele yake andika namba yake anayovalia mgongoni na mbele yake tena weka hashtag ya ‪#‎AzamFCPlayerOfSeason‬
Mfano: Abducado Emmanuel 19 #AzamFCPlayerOfSeason
Baada ya kufanya hivyo utakuwa umemaliza kupiga kura yako bila kuharibika, ila kumbuka kuwa hautaruhusiwa kupiga kura mara mbili au kuwapigia kura wachezaji wawili.
WACHEZAJI WALIOBAKIA KWENYE SITA BORA
*Shomari Kapombe- Jezi namba 4
*Aishi Manula- Jezi namba 28
*Pascal Wawa- Jezi namba 5
*Himid Mao- Jezi namba 23
*Farid Mussa- Jezi namba 17
*Ramadhan Singano- Jezi namba 14
N.B: Zoezi hili la kupiga kura litadumu hadi Jumatano ijayo Juni 15 kabla ya mshindi aliyejizolea kura nyingi kutangazwa.

Post a Comment

 
Top