KRZYSZTOF, baba yake staa wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Poland, Robert Lewandowski aliyefariki mwaka 1995, alikuwa mchezaji wa judo. Hata hivyo, familia hiyo haijaishiwa watu wanaojua mapigano, kwani mke wa Lewandowski, Anna Lewandowska, ni mpiganaji wa karate wa kiwango cha juu na usijaribu kumchokoza, utaumbuka, hata kama una mwili jumba namna gani.

 Anna ana jina kubwa kwenye karate duniani, kwani mwaka 2009, alitwaa medali ya shaba kwenye Kombe la Dunia la Karate. Utamchezeaje mrembo huyo? Yeye na Lewa walioana Juni 22, 2013.

Post a Comment

 
Top