SIMBA
ipo katika harakati za kuwasajili mabeki wa Prisons, Salum Kimenya na Nurdin
Chona, wote wawili wameapa kwamba kama dili lao likikamilika basi utakuwa
mwisho wa mastraika wa Yanga, Amissi Tambwe na Donald Ngoma kuipenya ngome ya
timu hiyo.
Simba inataka kuuongezea nguvu ukuta wake na
Kimenya na Chona wamethibitisha kwamba, kweli wamepigiwa simu za kuweka
mazingira ya kusajiliwa na timu hiyo.
Wakizungumza na Championi Jumamosi,
wachezaji hao walisema wapo katika mazungumzo na Simba ili waweze kusajiliwa na
wana matumaini mambo yataenda sawa.
“Ni kweli Simba nazungumza nao lakini bado
hatujafikia hatua ya mwisho, naamini nikisajiliwa nitajituma kuitumikia timu
yangu,” alisema Chona.
Alipoulizwa kuhusu kukumbana na Ngoma na Tambwe,
Chona alisema: “Nakuhakikishia nitapambana nao na nitaongeza mazoezi kwa ajili
yao, naamini hawatapita kwangu.”
Naye Kimenya alisema: “Nipo katika mazungumzo na
Simba, mambo yakiwa sawa nitakueleza. Kuhusu Ngoma na Tambwe binafsi nimewahi
kucheza nao na kweli wapo vizuri lakini nikiwa Simba naamini hawatanisumbua,
nitaongeza mazoezi binafsi kwa ajili yao.”
Akizungumza na Championi Jumamosi kuhusu
ujio wa mabeki hao, Tambwe alisema: “Hakuna beki wa kuninyima usingizi hapa
Tanzania, waache waongee tutakutana uwanjani.”
CHANZO: CHAMPIONI
Post a Comment