RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka
Ulaya (Uefa), Michel Platini amesema anatarajia rekodi yake ya ufungaji
ikavunjwa katika michuano ya Euro 2016 iliyoanza jana Ijumaa.
Platini, 60, ana rekodi ya kufunga
mabao tisa katika mechi tano za michuano ya Euro 1984 iliyofanyika Ufaransa.
"Rekodi yangu inaweza
kuvunjwa," alisema Platini na kuongeza: "Iliwekwa ili ivunjwe,
naamini wachezaji wapo vizuri kuivunja wakati huu japokuwa imechukua uda
mrefu.”
ZLATAN |
Kauli hiyo ya Platini inatokana na
uwepo wa Cristiano Ronaldo wa Ureno na Zlatan Ibrahimovic wa Sweden ambao wana
uwezo mkubwa wa kufunga. Katika Ligi Kuu Hispania ‘La Liga’, Ronaldo aliifungia
Real Madrid mabao 35 na Ibrahimovic yeye ameifungia PSG mabao 38 katika Ligi ya
Ufaransa ‘Ligue 1’.
Post a Comment