Baada ya kumalizika kwa ligi kuu ya Vodacom Tanzania
bara 2015/16 na Mbeya City fc kumaliza ikiwa kwenye nafasi
ya 8 baada ya kuweka kibindoni jumla ya Pointi 35, kufuatia
mabao 32 ya kufunga na kufungwa 34 kwenye michezo 30
ya msimu mzima.
Rekodi kadhaa kutoka bechi la ufundi zimetoka
na kati ya hizo baadhi
zinaonyesha kuwa, magolikipa watatu wa kikosi cha kwanza, Juma Kaseja,
Haningtony Kalyesubula na Geoffrey Mwalyego
waliokuwa wakisimama langoni kwa
kupishana kwenye michezo tofauti wamewajibika kwa asilimia 33.33 katika
ushindi, sare na hata kupoteza mchezo katika mechi zote 30 za msimu.
Katika rekodi hizo zinaonyesha, Juma
Kaseja alicheza michezo 17 na
kuruhusu kufungwa mabao 20, Haningtony Kalyesubula alicheza michezo 13 na
kufungwa mabao 14 wakati Geoffrey Mwalyego yeye hakupata nafasi ya kucheza
mchezo hata mmoja.
Wakati Mlinzi Hassan Mwasapili akiweka rekodi ya kucheza
mechi nyingi zaidi kikosini kuliko mchezaji yoyote kwa kucheza mechi 28 na
kukosa 2 pia kufunga mabao 2 katika mechi zote 30, Mlinzi wa kati Haruna
Shamte amemaliza akiwa na rekodi ya kupata kadi nyingi zaidi kuliko mchezaji
yoyote akiwa na jumla ya kadi 8, kati ya
hizo 6 zikiwa za njano na 2 nyekundu.
Kiungo Rafael Daud ndiye kinara wa mabao kikosini akimaliza
msimu kwa kufunga mabao 6,na kuifikia rekodi ya Mwegane Yeya aliyoiweka
2013/14, ingawa pia
ukurasa wake ukionyesha kuwa alipata kadi 2 za njano.
Mlinzi na kiungo Aboubakary Shaaban akiweka rekodi ya
kucheza ligi kuu akiwa na umri mdogo zaidi kuliko wachezaji wote wa City,
akicheza mechi yake ya kwanza dhidi ya Coastal Union jijini Tanga akiwa na umri
wa miaka 17 na siku 129.
David Kabole alicheza mechi 1 na kufunga bao 1 hii ilikuwa
kwenye mchezo dhidi ya JKT Ruvu ambao City ilipata ushindi wa 3-0 lakini baada
ya hapo hakuonekana tena dimbani hii ni
baada ya kiwango chake kuporomoka kwa kasi na kujikuta akitolewa kwa mkopo kwenda
Fc Kimondo na kumpisha Salvatory Nkulula
aliyeingia kikosini na kufanikiwa kucheza mechi 6 akifunga mabao 4.
Rekodi pia
zinaonyesha 2015/16 ndiyo msimu
pekee ambao City imekuwa chini ya makocha watatu, ikianza na Juma
Mwambusi aliyeondoka baadae, na nafasi yake kushikwa na Abdul
Mingange ambaye alidumu kikosini kwa miezi 3, kufuatia
matatizo ya kifamilia Mingane aliachia
nafasi hiyo na kumpisha kocha wa sasa Kinnah Phiri.
Licha ya kushinda 4-0 dhidi ya Coastal Union kwenye mchezo
wa duru ya pili April 4 kwenye uwanja wa Sokoine jijini hapa, ushindi mkubwa wa
City msimu huu ulikuwa ni ule wa bao 5-1 dhidi ya Toto Africans katika mechi ya
kukata nashoka iliyopigwa jijini Mbeya, huku kipiko kikali kikiwa ni kile cha
mabao 4-1 ilichokipa kutoka kwa Ndanda Fc huko Nangwanda Sijaona.
Katika nyota walisajiliwa wakati wa dirisha dogo Haruna
Moshi ameonekan kung’ara zaidi
akifanikiwa kumaliza msimu akiwa amefunga mabao 3, sambamba na Ramadhani
Chombo,Abdalah Juma na Ditram Nchimbi
waliofunga 2 kila mmoja ingawa Abdalah Juma hakumudu kuitumikia timu kwa
kiwango kutokana na majereha ya mara kwa mara.
2015/16 ndiyo msimu pekee ambao City imeshinda mechi mbili
pekee ugenini, 2-1 dhidi ya Jkt Ruvu
Karume Dar na 1-0 dhidi ya Mgambo JKT,
Mkwakwani, Tanga, huku pia
ikivuna pointi 3 za sare ugenini dhidi
ya Toto Africans, Coastal Union na Mwadui Fc.
Post a Comment