OBERHAUSEN, Ujerumani
KLABU ya Rot-Weiss Oberhausen ya Ujerumani
imemwambia nyota aliyemaliza mkataba wake PSG, Zlatan Ibrahimovic kwamba:
“Ukikubali kujiunga na timu yetu tunakupa ufalme wa mji wetu.”
Rot-Weiss Oberhausen inashiriki Ligi
Daraja la Nne Ujerumani ikiwa inafundishwa na Kocha Andreas Zimmerman, inatumia
Uwanja wa Niederrheinstadion unaoingiza mashabiki 21,318.
Klabu hiyo imeweka katika mtandao wake
baadhi ya makubaliano ya mkataba mpya kama Ibrahimovic atakubali kujiunga nao
ni kwamba, atapewa ufalme wa mji wao.
Pia watamjengea bwawa la kuogelea la
kienyeji popote atakapotaka na jina lake litatumika kama jina la bia yao, yaani
wataiita ‘Ibrahimovic Beer’.
“Kama Ibrahimovic atakubali kujiunga
nasi, tutampa ufalme wa mji wetu pia jina lake tutalitumia kuiita pombe yetu ya
kienyeji,” ilisema sehemu ya taarifa yao
Ibrahimovic raia wa Sweden amemaliza
mkataba wake na PSG akiwa ameifungia mabao 156 katika mechi 180.
Post a Comment