BAADA ya Yanga kumsajili beki wa kulia wa Simba, Hassan
Kessy, Mrundi, Karim Nzigiyimana wa Gor Mahia amesema yupo tayari kutua
Msimbazi kuchukua nafasi ya Kessy.
Kama ilivyo kwa Kessy, Nzigiyimana naye anamudu kucheza
nafasi ya beki wa kulia na anasisitiza kamwe Simba haitajuta ikimsajili.
Nzigiyimana ambaye ni kiraka mwenye uwezo wa kucheza nafasi
nyingi uwanjani isipokuwa langoni, alijiunga na Gor Mahia mwaka 2011 akitokea
Rayon Sport ya Rwanda.
Akizungumza kutoka Burundi, Nzigiyimana alisema, amesikia Kessy
ameondoka Simba, hivyo anataka kuchukua nafasi yake ili kutimiza ndoto yake ya
muda mrefu ya kucheza soka Tanzania.
“Nimesikia Kessy ameondoka Simba sasa nipo tayari kuja kuchukua
nafasi yake kwa sababu nimebakisha mkataba wa miezi sita na Gor Mahia, Kessy ni
mchezaji mzuri ambaye tunafanana katika kucheza
sasa naamini kama Simba wakinifuata itakuwa vizuri.
“Sijazungumza na Gor Mahia hadi sasa kwani nadhani umefika
wakati wa kucheza nje ya Kenya na chaguo langu la kwanza ni Tanzania na kwa
kuwa Simba imeachana na Kessy, nataka kwenda hapo,” alisema Nzigiyimana.
Beki huyo alisema anaamini ligi ya Tanzania ni bora na
atacheza kwa ushindani mkubwa endapo atapata nafasi ya kucheza Simba.
CHANZO: CHAMPIONI
Post a Comment