Dar es Salaam
STRAIKA Mbwana Samatta wa KRC Genk amesema Yanga kama
ikijipanga inaweza kuifunga TP Mazembe katika mechi yao ya hatua ya makundi ya
Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga itacheza na TP Mazembe ya DR Congo kati ya Juni 28 na
29, mwaka huu jijini Dar es Salaam mchezo wa kwanza wa Kundi A la Kombe la Shirikisho.
Samatta aliyewahi kuichezea TP Mazembe akitokea Simba,
ameliambia Championi Jumamosi kuwa, Yanga inaweza kuiondoa TP Mazembe katika michuano hiyo kama
ikijipanga ipasavyo.
Alisema anaamini hilo linawezekana kwani kikosi cha Yanga
hivi sasa kipo vizuri ukilinganisha na misimu mingine iliyopita.
“Hali hiyo ndiyo
inayonifanya niamini kuwa Yanga inaweza kuifunga TP Mazembe, kwani nimekuwa
nikiifuatilia sana na kuona jinsi wachezaji wake wanavyopambana uwanjani.
“Hata hivyo Yanga wanatakiwa kujipanga na kukiandaa kikosi
chao kwa ajili ya michuano hiyo, kama kuna upungufu ambao waliuona hapo awali
basi muda huu ndiyo wa kuufanyia kazi kabla ya kuanza kwa hatua hiyo makundi.
“TP Mazembe ni timu nzuri na yenye mafanikio Afrika, lakini
katika soka lolote linaweza kutoka ndiyo maana nimesema Yanga inaweza kuifunga
timu hiyo kama ikijiandaa vizuri,” alisema Samatta ambaye leo ataichezea Taifa
Stars dhidi ya Misri.
CHANZO: CHAMPIONI
Post a Comment