KOCHA wa Ureno, Fernando Santos uwepo
wa Cristiano Ronaldo katika kikosi chao kwenye michuano ya Euro 2016,
kumeongeza hatari ya kiusalama hasa mashambulizi ya kigaidi.
Santos amesisitiza kuwa, Ureno
inahitaji ulinzi zaidi katika michuano hiyo kwani ndiyo inayoweza kuwindwa
zaidi kushambuliwa kutokana na uwepo wa Ronaldo anayechezea Real Madrid ya
Hispania.
"Ureno ni moja ya timu zilizo
kwenye hatari kubwa, kwa sababu tunaye Cristiano Ronaldo. Tumejiandaa kwa hali
hiyo," alisema Santos nakuongeza:
"Tunajua maofisa usalama wa
Ufaransa wanajua hilo na watakuwa makini kuhusu usalama wetu maana vitu vingine
vya usalama ni nje ya timu binafsi.
"Lakini hatuogopi, familia ya
soka lazima ichukulie ukubwa wa jambo hili. Lazima tueleze ukweli ili tuone
mamlaka zinavyofanya kazi.”
Post a Comment