WAKATI Lionel Messi akisema hakuwa akisoma mikataba aliyosaini na kutupa mpira kwa baba yake, mzazi wake huyo amesema alifanya yote hayo ili kumweka mwanaye katika maisha mazuri.
Messi anakabiriwa na kesi ya ukwepaji kodi na tayari ameshasema kuwa, mara nyingi anasaini mikataba bila ya kufahamu kilichomo akiamini kazi hiyo inafanya na wasaidizi wake akiwemo baba yake.
Baba wa Messi, Jorge Messi alisema mahakamani kuwa, mtoto wake hana hatia kama alivyosema isipokuwa watu wake wa sheria ndiyo waliosababisha mambo kwenda ilivyo sasa.

“Yeye anachojua ni kucheza soka tu na siyo mambo mengine sasa tunahitaji msaada wa kisheria na mambo ya hesabu ili kuepuka mambo haya,” alisema Jorge.
Hoja ya msingi ya Messi na baba yake ni kwamba, mambo yao yote kisheria na biashara yapo chini ya Juarez & Associates na Rodolfo Schinocca.
"Schinocca alifanya mkataba wa kwanza na tukaamimi kila kitu kipo sawa, pia kama mdhamini ana kitu cha ziada watu wa Juarez & Associates hunieleza, hivyo sikuwa na wasiwasi.”
Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea tena jana Ijumaa kwa hatua zaidi.

Post a Comment

 
Top