Kocha wa Misri Hector Cuper amesema licha ya ushindi wa mabao
2-0 dhidi ya Tanzania lakini amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na
mshambuliaji wa Taifa Stars Mbwana Samatta.
Cuper raia wa Argentina ameiambia Tanzaniabettingarena,
amevutiwa sana na kiwango cha Samatta na huenda akaja kuwa msaada mkubwa kwa
Tanzania siku zijazo kama atapata nafasi ya kucheza kwa muda mrefu KR Genk
anapocheza hivi sasa.
“Nimchezaji mwenye jipaji kikubwa cha soka na nimsaada mkubwa
kwa Tanzania lakini hakuweza kungara kutokana na timu yangu nilivyoipanga na
mahitaji tuliyokuwa tunayataka,”amesema Cuper.
Kocha huyo alisema kukosa penati ni jambo la kawaida kwenye
mchezo na mchezaji yeyote anaweza kufanya hivyo lakini pamoja na hivyo Samatta
anabaki kuwa bora kwenye kikosi cha Tanzania
Post a Comment