STAA wa Bongo, Nasibu Abduli ‘Diamond
Platinumz’ ana kesi kwa mashabiki wake.
Ijumaa na Jumamosi hii wamekuwa wakisubiri kwa hamu video ya wimbo wake
aliowashirikisha P-Square ambayo aliahidi ingetoka jana, lakini hadi sasa
kimya!!
Wengi wameonesha kukusa
uvumilivu na wameanza kuelezea kusikitishwa kwao kwenye akaunti zake za
mitandao ya kijamii.
Lakini tumeongea na uongozi wake
kutaka kujua nini sababu za kuchelewa kutoka kwa video hiyo, na umesema kuwa
kuna vitu vichache vimechelewesha na kwamba mashabiki wasiwe na shaka kwasababu
kiu yao itakatwa.
“Kuna vitu vinachelewesha ila
tupo katika final touches,” meneja wa Diamond, Sallam ameiambia blog hii.
“Ukiwapa kitu kibaya
watalalamika ni bora wafanye subira wapate kizuri zaidi,” ameongeza.
Video ya wimbo huo ilifanyika
nchini Afrika Kusini na utakuwa wimbo wa kwanza P-Square wanasikika wakiwa
pamoja tangu kundi lao kudaiwa kuvunjika.
Ijumaa hii Diamond alipost
kwenye Instagram picha ya mwanae Tiffah mwenye umri wa miezi 11 sasa na
kuandika: On the LONG conversation with my Miss World before Making a History.”
Ujumbe huo uliwapa matumaini
mashabiki wake kuwa muda wa kuiona video hiyo umekaribia.
CHANZO: Bongo 5
Post a Comment