April 11, 2025 10:34:26 PM Menu




 KOCHA mpya wa Manchester United, Jose Mourinho amekataa kusaini jezi ya Chelsea baada ya kutakiwa kufanya hivyo na shabiki nchini China.
Mourinho ambaye yupo na timu yake katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya alikuwa mwenye furaha wakati akisaini jezi za mashabiki mbalimbali wa timu yake hiyo ndipo ghafla akatokea shabiki mmoja akiwa na jezi ya Chelsea na kupanga foleni akitaka naye asainiwe jezi yake.

Kabla hata ya Mourinho kumfikia shabiki huyo, mlinzi mmoja alianza kumsukuma ili asogee pembeni, ilipofika zamu ya shabiki huyo Mourinho alimpotezea huku akionekana kuwa na tabasamu dogo.

Mourinho alikuwa kocha wa Chelsea kwa vipindi viwili tofauti kabla ya kutua Man United, mara ya mwisho aliondoka Chelsea kwa kufukuzwa mwaka jana baada ya timu hiyo kuwa na matokeo mabaya.




23 Jul 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top