April 11, 2025 09:37:16 AM Menu




HII ni kufuru, kipaji kinalipa asikuambie mtu. Ureno wameamua kumfanyia kufuru straika wao Cristiano Ronaldo baada ya kuamua uwanja wa ndege kupewa jina lake kufuatia kuwawezesha kubeba ubingwa wa Euro hivi karibuni.
Uwanja wa ndege wa nyumbani kwao  Madeira ujulikanao kama International Santa Catarina Airport, sasa utajulikana kwa jina la Cristiano Ronaldo International Airport. Hiyo ni kwa ajili ya kutambua mafanikio ambayo mkali huyo ameyapata katika soka.
Hii sasa inamaanisha jina la Ronaldo linazidi kwenda juu zaidi ya hata ya la mpinzani wake, Lionel Messi.

Tangazo hilo la uwanja kupewa jina la Ronaldo, lilitamkwa na Rais wa Serikali ya Mkoa wa Madeira, Miguel Albuquerque siku ambayo Ronaldo alipaa kwenda Funchal kuifungua hoteli yake ya Pestana CR7.
Tayari katika mji huo kuna sanamu ya Ronaldo ambayo inatumika kama kivutio cha watalii.
25 Jul 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top