April 11, 2025 04:17:42 AM Menu



KIUNGO wa zamani wa Arsenal, Mikel Arteta, 34, amefuta picha zote alizokuwa ametinga uzi wa timu hiyo baada ya kujiunga na Man City akiwa katika jopo la makocha chini ya Pep Guardiola.
Kiungo huyo ambaye alijiunga na Arsenal miaka mitano iliyopita, amefanya tukio hilo kwenye mtandao wa Instagram ambapo mashabiki wa Gunners walikuja juu na kumpa maneno makali kwa kitendo hicho.
Arteta sasa anaonekana kuingia kwenye kundi la ‘wasaliti’ wa Arsenal kama walivyofanya makapenti waliopita ambao ni, Cesc Fabregas na Robin van Persie.
Baadhi ya komenti za mashabiki hao zilisema:
“Arteta amefuta picha zote za Arsenal kwenye Instagram, namfuta Arteta kwenye moyo wangu.”
 “Arteta alicheza kwa sekunde 30 msimu uliopita na alihusika ‘kutukosti’ kwenye mechi mbili, nina matumaini Arsenal itafanya kama alivyofanya yeye kwa kufuta historia yake yote.”
Account ya Arteta ambayo anatumia jina la mikelarteta ina wafuasi 201k na ina picha mbili tu akiwa na jezi ya timu nyingine.
25 Jul 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top