April 12, 2025 10:18:14 AM Menu



YANGA ilipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Medeama ya Ghana, timu hizo zinatarajiwa kurudiana Jumanne ijayo lakini habari kubwa kwa Waghana hao ni kuwa wanaweka mikakati ya kuwadhibiti washambuliaji wawili wa Yanga, Donald Ngoma na Obrey Chirwa.

Straika wa Medeama, Bismark Oppong, amesema Yanga ni timu nzuri lakini wamebaini kuwa wanabadilika zaidi pale mpira unapokuwa kwa mastraika wao hao hivyo watajizatiti kuwazuia ili wasiwaletee shida wakiwa kwao.

“Ni kweli Yanga ni wazuri sehemu nyingi lakini mastraika wao wawili, yule Ngoma na aliyevaa namba 7 (Chirwa) ni wazuri sana. Hao ndiyo tunaotakiwa kucheza nao sana katika mechi yetu ya marudiano, hatutaki watusumbue Ghana, tukiwazuia hao, tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa,” alisema Bismark.

Ukiachana na usumbufu aliouonyesha Ngoma katika mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho iliyochezwa Julai 16 jijini Dar, bao la Yanga lilifungwa na Ngoma wakati lile la wageni liliwekwa wavuni na Bernard Danso.
Timu hizo zitarudiana kwenye Uwanja wa Sekondi-Takoradi.
22 Jul 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top