April 11, 2025 03:23:23 PM Menu



 
Mkuu wa Azam, Zeben Hernandez, raia wa Hispania, amesema kiwango kinachoonyeshwa na straika Mzimbabwe, Bruce Kangwa, kinamfanya asite kukataa kumpa ulaji kikosini hapo.
Kangwa ambaye ametokea nchi moja na straika wa Yanga, Donald Ngoma kwa sasa anafanya majaribio ya kupata nafasi ya kuichezea Azam kwa msimu ujao, ametokea timu ya Highlander ya nchini kwao na tayari ameshacheza mechi mbili za kirafiki ilizocheza Azam kati ya zile tatu.

Mzimbabwe huyo alitua nchini Jumanne iliyopita, kesho yake akacheza mechi ya kwanza dhidi ya Friends Ranger ambapo Azam ilishinda 2-1, kisha juzi Jumamosi akacheza tena dhidi ya Mshikamano na Azam tena kuibuka na ushindi wa mabao 5-0.
Baada ya kumuona katika mechi hizo mbili, Zeben alisema: “Huyu jamaa ni mchezaji mzuri na akiendelea hivihivi, nadhani tutakuwa naye kwa msimu ujao kwani ana kila sababu za kunifanya nimjumuishe kikosini kwangu.”


25 Jul 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top