April 10, 2025 09:12:51 PM Menu




STAA wa mpira wa kikapu katika Ligi ya NBA, Stephen Curry amesema kuwa hakufurahishwa kutokuwemo katika kikosi cha taifa lake la Marekani kitakachoshiriki kwenye Michezo ya Olimpiki, mwezi ujao.

"Sikufurahishwa kabisa kukosa michezo hiyo, nilitamani sana kupata nafasi hiyo ya kucheza lakini majeraha niliyoyapata katika mechi za mtoano yalibadili kila kitu,” alisema mchezaji huyo wa Golden State Warriors. 

"Nilijua nitapona ndani ya muda mfupi, lakini mambo yalikuwa tofauti, nilizungumza na Kocha K (Mike Krzyzewski) na Colangelo (Jerry Colangelo, Mkurugenzi wa Mpira wa Kikapu Marekani) na kuwaomba wanipe muda, kilichotokea kikawa tofauti, ikabidi nikubali ili nipate muda wa kupumzika kujiandaa na msimu mpya," alisema Curry. 



23 Jul 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top