SIMBA SC imemaua – baada ya
kuingia Mkataba na kocha Mcameroon Joseph Marius Omog sasa imehamia kwenye
kusajili wachezaji bora wa kigeni.
Wakati tayari ikiwa imefikia
makubaliano na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Laudit Mavugo aje kusiani
Mkataba wa miaka miwili, Simba SC inaleta mshambuliaji hatari kutoka Ivory
Coast.
Huyo ni Goue Frederic Noel
Blagnon aliyezaliwa Desemba 26, mwaka 1985 ambaye anatokea klabu ya African
Sports ya kwao, Ivory Coast.
Mchezaji huyo wa zamani wa Union
Sportive de Bitam ya Gabon na Asante Kotoko ya Ghana, anakuja Simba SC kwa
msaada wa kipa Muivory Coast wa timu hiyo, Vincent Angban.
Blagnon anayependa kuvaa jezi
namba 11, anatarajiwa kuwasili usiku huu pamoja na kipa Angban na Jumatatu
anaweza kuwa mazoezi Simba SC, ili kwanza kocha Omog amuone na kujiridhisha juu
ya uwezo wake.
Omog alisaini Mkataba wa miaka
miwili Ijumaa, ikiwa ni siku moja baada ya kuwasili nchini na anarithi mikoba
ya
Muingereza Dylan Kerr
aliyetimuliwa mapema mwaka huu na nafasi yake kukaimishwa Mganda Jackson
Mayanja.
Ingawa Simba SC inataka Mayanja
aendelee na kazi kama Msaidizi wa Omog, lakini hakuna uhakika kama hilo
litawezekana na tayari taarifa zisizo rasmi zinasema Mganda huyo anataka
kurejea Kagera Sugar.
Simba SC inatarajiwa kuanza
mazoezi Jumatatu na wachezaji kadhaa wapya wanatarajiwa kuhudhuria ili
kufanyiwa majaribio.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.