KOCHA
mpya wa Simba, Joseph Omog amesema yeye sera ya soka lake analolitaka ndani ya
uwanja ni lile la pasi siyo mashambulizi ya ghafla yaani ‘kaunta ataki’ na
anaamini atafanikiwa kwa pasi zake.
Wakati
kocha huyo akitaka soka la pasi kama linalochezwa na Arsenal ya England,
wapinzani wao Yanga wenyewe chini ya kocha wao Mholanzi, Hans van Der Pluijm
wanacheza soka la kasi linalotegemea mashambulizi hayo ya kushitukiza.
Omog
raia wa Cameroon, aliwasili nchini usiku wa kuamkia juzi akitokea kwao na jana
mchana alisaini mkataba wa miaka miwili kuifundisha Simba hadi mwaka 2018.
Akizungumza
na Championi Jumamosi, Omog alisema sera yake kubwa ni timu yake kucheza
soka la pasi nyingi za haraka wakati wakiwa na mpira wakienda kushambulia lango
la timu pinzani.
Omog
alisema, anaifahamu vizuri Simba ambayo aliwahi kukutana nayo mara mbili kwenye
msimu wa 2013/14, hivyo ana matumaini makubwa ya kuleta mabadiliko katika msimu
ujao wa Ligi Kuu Bara.
Kila
kocha ana sera yake katika timu, lakini kwa upande wangu mimi ninataka kuona
timu yangu ikicheza soka la pasi nyingi wakati timu ikiwa na mpira tukiwa
tunashambulia.
“Pia
wakati timu ikiwa bila mpira, ninataka kuona wachezaji wangu wakikaba wote na
hilo ndilo soka la kisasa hivi sasa, ninataka kuona tunacheza kitimu,” alisema
Omog aliyewahi kuinoa Azam na kuipa ubingwa wa ligi kuu msimu wa 2014/15.
Post a Comment