KUNA
dili la straika wa Yanga, Donald Ngoma kusajiliwa na Mamelodi Sundown ya Afrika
Kusini, sasa klabu yake imeelezwa kuanza harakati za kuziba nafasi yake kwa
kumtaka Kipre Tchetche wa Azam FC.
Ngoma
aliyetua Yanga msimu uliopita kwa kusaini mkataba wa miaka miwili na kufanya
vizuri ameivutia Mamelodi ambayo imeapa kumsajili ili akaisaidie katika Ligi
Kuu ya Afrika Kusini.
Mmoja
wa mabosi wa Yanga mwenye nguvu kubwa ya ushawishi katika mambo ya usajili
aliliambia Championi Jumamosi kuwa, kutokana na Mamelodi kuongeza nguvu
ya kumuhitaji Ngoma na wao wanazungumza na Azam ili wamsajili Tchetche raia wa
Ivory Coast.
Alisema
lengo lao ni kupata msaada wa Tchetche katika mechi za kimataifa na msimu ujao
wa Ligi Kuu Bara.
“Tumewafuata
Azam ili waweze kutukubalia kumsajili Tchetche ambaye bado ana mkataba wa mwaka
mmoja nao, kuna masharti wametupa ili kufikia makubaliano.
“Tunataka
Tchetche achukue nafasi ya Ngoma kwani kuna uwezekano mkubwa akaondoka hivyo
hatutaki kupata tabu pia tunazungumza kuhusu uwezekano wa kumsajili na Pascal
Wawa.
![]() |
KIPRE |
“Ila
kuhusu Wawa bado tunavutana kwani itabidi tumuache mchezaji mwingine au iwe kwa
makubaliano maalum ya mechi za kimataifa tu, naamini Azam watakubali kwa faida
ya nchi.
Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka
Deusdedit alisema: “Bado mapema sana kuzungumzia suala hilo, mimi sijui
inawezekana watu wa usajili ndiyo wanafahamu zaidi.”
Lakini Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassor
kuhusu suala hilo, alisema: “Kwa upande wetu hatuwezi kuwazuia Yanga kuja
kumsajili Tchetche kwani soka ni mchezo
wa furaha.
“Tunawakaribisha Yanga kama wanamuhitaji
Tchetche tukae mezani wamsajili lakini kwa sasa hatujaona barua yao yoyote na
iwapo hawatakuja basi ataendelea kuitumikia Azam.”
Post a Comment