Kesho ndiyo Kocha Joseph Omog anaanza rasmi kazi yake ya
kuinoa timu yake mpya ya Simba.
Omog ametaka wachezaji wote waliosajiliwa Simba au
wanaotarajia kusajiliwa wawe mazoezini bila kukosa.
Omog raia wa Cameroon, ameuambia uongozi angetaka kumuona
kila mchezaji wa Simba akiwa mazoezini.
"Kocha anachotaka ni kila mchezaji wa Simba kuwa
mazoezini kesho Jumatatu. Anataka kuwaona wachezaji wote bila ya kukosa na kama
akianza, aanze moja kwa moja," kilieleza chanzo.
Omog aliwahi kuinoa Azam FC na kuipa ubingwa wa Tanzania
Bara mwaka 2014, timu hiyo ilichukua ubingwa bila kupoteza mechi hata moja.
CHANZO:
salehjembe
Post a Comment