CALIFORNIA,
Marekani
MCHEZAJI
wa kikapu, DeMar DeRozan ambaye kwa sasa ni mchezaji huru, imeelezwa kuwa
amekubali kurejea kwenye timu ya Toronto Raptors na kusaini mkataba wa miaka
mitano wenye thamani ya dola milioni 139.
DeRozan
alikuwa katika timu hiyo inayoshiriki ligi ya kikapu ya NBA tangu mwaka 2009
lakini alimaliza mkataba na kuwa mchezaji huru baada ya msimu wa 2015/16
kufikia tamati lakini kuna uwezekano mkubwa wa kurejea katika timu hiyo.
Msimu
uliopita DeRozan alikuwa na wastani wa pointi 23.5 katika mechi 78 alizocheza.
Toronto
haikuwa na msimu mzuri japokuwa ilifika hatua ya fainali ya Ukanda wa Mashariki
na kutolewa na Cleveland Cavaliers ambao baadaye walifanikiwa kuwa mabingwa.
Taarifa
zinasema kuwa DeRozan atatambulishwa rasmi Julai 7, mwaka huu kuwa mchezaji wa Raptors.
Post a Comment