PARIS,
Ufaransa
BEKI
wa timu ya taifa ya Ufaransa, Patrice Evra amesema kuwa wao watakuwa makini na
hawataidharau Iceland kama ilivyotokea kwa England katika michuano ya Euro
inayoendelea.
Ufaransa inatarajiwa kucheza dhidi ya Iceland, leo
Jumapili katika nusu fainali ya michuano hiyo huku wengi wakiipa nafasi
Ufaransa kupata ushindi. Iceland walifika hatua hiyo baada ya kuifunga England
mabao 2-1 katika robo fainali, wiki iliyopita.
Beki huyo wa zamani wa Manchester United amesisitiza kuwa
England hawakuiheshimu Iceland na ndiyo maana wakapoteza mchezo huo.
“Inanipa
hofu kwa kuwa England hawakuiheshimu Iceland kwa kuwa watu wengi wanadharau
mataifa madogo,” alisema beki huyo mwenye umri wa miaka 35.
“Kilichotokea
England walitakiwa kushinda lakini kwa kawaida unapoingia katika mchezo
unatakiwa ujiwekee asilimia 50-50.
“Mara
baada ya mechi yetu dhidi ya Ireland kuna Waingereza wakawa wananiuliza juu ya
mimi kukutana na England lakini nikawajibu kuwa chochote kinaweza kutokea
katika mchezo wao na Iceland lakini hawakulijali hilo,” alisema Evra
Post a Comment