MPAKA kitaeleweka
tu, kwani sasa Simba imethibitisha ujio wa mshambuliaji wao mpya waliyekuwa
wakimsaka kwa muda mrefu, Laudit Mavugo atakuja nchini keshokutwa Jumatatu.
Simba msimu uliopita ilikwama kumsajili Mavugo
kwani haikuweza kukubaliana bei na timu yake ya Vital’O ya Burundi licha ya
kutanguliziwa fedha, lakini sasa mambo yanaonekana kuwa ‘fresh’.
Kwa siri sana, mmoja wa mabosi wa Kamati ya
Usajili ya Simba, amelinyetishia
Championi Jumamosi kuwa, mipango ya kumleta Mavugo bado ipo palepale na
anatarajiwa kutua nchini Jumatatu ijayo tayari kwa kujiunga na timu yao.
“Vital’O wameamua kumjumuhisha Mavugo katika
kikosi huku wakijua mchezaji huyo amemaliza mkataba na kudai kuwa straika huyo
ni mali ya Simba kwa sasa.
“Mavugo tayari aliingia mkataba kwa dau la Sh
milioni 36 tangu msimu uliopita, tunatarajia atakuja Jumatatu, ataingia kambini
na timu kati ya Zanzibar au Morogoro,” alisema bosi huyo.
Post a Comment