STRAIKA mpya wa
Yanga, Obrey Chirwa raia wa Zambia, ameendeleza kutishia uhai wa pacha ya
Donald Ngoma na Amissi Tambwe huku akisaka namba ya mmojawapo msimu ujao
kutokana na uwezo mkubwa anaouonyesha kwenye mazoezi ya kikosi hicho.
Nyota huyo wa zamani wa FC Platinum ya
Zimbabwe, jana aligeuka gumzo kwa mashabiki waliokuwa kwenye mazoezi ya Yanga
baada ya kufunga bonge la bao la kichwa cha mkizi, kama alilowahi kufunga Robin
van Persie wa Uholanzi katika Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil.
![]() |
VAN PERSIE AKIFUNGA BAO LINALOFANANISHWA NA ALILOFUNGWA CHIRWA |
Chirwa alifunga bao hilo kwenye mazoezi ya
kikosi hicho yaliyofanyika Uwanja wa Boko Veterani, Dar ambako Yanga inajiandaa
na mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, hatua ya makundi dhidi ya Medeama.
Championi Jumamosi lililokuwepo mazoezini hapo, lilishuhudia
Chirwa ‘akielea’ angani kuunganisha kwa kichwa krosi ya winga machachari, Simon
Msuva katika mazoezi ambayo Kocha Hans van Der Pluijm aliigawa timu katika
vikosi viwili.
Ajabu baada ya kuingia kwa bao hilo, mashabiki
walilipuka kwa shangwe na kuanza kumshangilia huku wakisema: “Ngoma jiandae kwa
moto huu wa Chirwa lazima kazi uwe nayo msimu ujao. Huyu jamaa ni noma aisee.”
Bado kuna kitendawili cha nani aanze kwenye
safu ya ushambuliaji kati ya Chirwa, Tambwe na Ngoma ambao kwa pamoja wamekuwa
wakiwakosha mashabiki kwa ubora wao.
Post a Comment