ARSENAL wako kwenye mazungumzo ya
kutaka kumaliza kabisa uhamisho wa wachezaji wawili wa mabingwa wa Premier
League Leicester kwa kumuulizia winga Riyad Mahrez, 25, achukuliwe pamoja na
mshambuliaji Jamie Vardy, 29.
(Chanzo Sun)
Washika Bunduki wa London wanaamini
kuwa Vard atatia saini kwenye klabu yao kabla ya kuanza kwa mashindano ya Euro
2016 siku ya Ijumaa. (Chanzo Telegraph)
Bado hayajatolewa maamuzi yoyote
kuhusu hatma ya Vardy. Mshambuliaji huyo ameahidiwa ofa ya kulipwa paundi
120,000 kwa wiki na washika Bunduki. (Chanzo Leicester Mercury)
Leicester wanamtizamia mshambuliaji wa
Watford Troy Deeney, 27, kama mbadala wa Vardy. (Chanzo Telegraph)
Kocha mpya wa Manchester City, Pep
Guardiola amepewa sifa na mwenyekiti wa klabu hiyo, Khaldoon Al Mubarak kuwa
ataibadilisha klabu hiyo na kuipeleka level nyingine. (Chanzo City TV)
Guardiola anatizamia kuimarisha zaidi
safu yake ya kiungo kwa kumsajili Toni Kroos, 26, kutoka Real Madrid, huku
Fernando, 28, akiwa anahitajika na klabu za La Liga Villareal na Valencia.
(Chanzo Manchester Eveing News)
Winga wa Chelsea Eden Hazard, 25,
ameondoa ule uvumi uliokuwa ukimuhusisha na kuhamia Paris St-Germain baada ya
kusema “PSG haiko kwenye mipango yangu sababu bado najisikia vizuri kuendelea kuitumikia Klabu yangu ya Chelsea”. Kiungo huyo anaonekana
kukubali kuendelea kufanya kazi na kocha mpya, Antonio Conte. (Chanzo Telefoot)
Klabu ya Chelsea imefungua mazungumzo
juu ya uhamisho wa Alvaro Morata kufuatia klabu ya Arsenal iliyokuwa ikimnyatia
nyota huyo pia kuonekana kuhamia kwa straika wa Leicester City, Jamie Vardy.
(Chanzo Telegraph)
PSG wanataka kumshawishi kiungo wa
Leicester N’Golo Kante, 25, kwa kumpatia ofa ya mkataba wa miaka mitano ili
aichezee timu yao msimu ujao. (Chanzo Daily Mirror)
Zlatan Ibrahimovic amewaambia
mashabiki wa Manchester United kuwa tamko lake kubwa ataliachia rasmi siku ya
kesho Jumanne. (Chanzo The Sun)
Kipa aliye kwenye kiwango katika
kikosi cha Manchester United, David de Gea, 25, kuna uwezekano akaendelea
kubaki Old Trafford baada ya Real Madrid kuamua kuachana na kulipa pauni
millioni 39 za kutengua kipengere cha kumnunua kwenye mkataba wake. (Chanzo AS)
Unataka tukuletee tena habari hizi
hapo kesho? Basi acha uchoyo, Gonga “LIKE” halafu “SHARE” na marafiki zako
wapenda soka waone habari hizi.
Post a Comment