May 3, 2025 08:59:48 PM Menu




KIUNGO wa zamani wa Simba, William Lucian ‘Galllas’ ameruhusiwa kujiunga Ndanda FC badala ya Mwadui FC baada kufutiwa adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufutia kusaini timu mbili kwa mpigo.

Gallas ambaye msimu uliyopita aliichezea Ndanda FC akitokea Simba kabla ya kuongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia timu hiyo katika ligi ya msimu lakini  aliamua kujiunga Mwadui kwa mkataba wa mwaka mmoja hali iliyosababisha kufungiwa mwaka moja kutocheza mpira na TFF.

Mwenyekiti wa Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza), Mussa Kisoki alisema: “Gallas tumefanikiwa kumnasua katika kifungo cha mwaka mmoja na atacheza ligi msimu akiwa na timu yake ya zamani Ndanda baada ya kufanyika makubaliano.”

Championi Ijumaa lilimtafuta kiungo huyo ambaye alisema anashukuru Mungu kutokana na kufanikiwa kutoka kifungoni huku akitakiwa kurejea Ndanda kutumikia mkataba wake wa mwaka mmoja alisaini awali tofauti na Mwadui. 
30 Sep 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top