May 8, 2025 04:11:01 PM Menu



 WAKATI Yanga wakitarajiwa kwena kwa ndege mkoani Shinyanga kupambana na Mwadui FC mwishoni mwa wiki, kocha mwenye maneno mengi, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ ameanza vitisho.

Wanajangwani hao ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, watacheza na Mwadui mchezo utakaochezwa Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga keshokutwa Jumamosi.
Julio ameiambia spotiripotablog kuwa hatishwi na Yanga hata kidogo kwani kikosi chake hicho cha Mwadui kimejipanga kuhakikisha kinawatoa nishai mabingwa hao watetezi.

“Sijawahi kutishika na timu hizo ambazo zinajiita kubwa, mimi najiamini na nina kiamini kikosi changu hivyo hao Yanga tunawakaribisha kwa mikono miwili.
 “Niseme tu kwamba, siwaogopi bali ninawaheshimu kama mabingwa watetezi, nadhani mnakumbuka hata msimu uliopita hawakuweza kutufunga hapa kwetu,” alisema.
Timu hizo zilipokutana msimu uliopita zilitoka sare ya ya mabao 2-2 kwenye Uwanja wa Kambarage.
15 Sep 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top