May 4, 2025 10:02:21 PM Menu



WAKATI wapinzani wa Yanga wakibeza kiwango cha Obrey Chirwa, baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wanaamini kuwa mchezaji wao huyo atawaumbua Wanamsimbazi hao watakapokutana.
Miamba hiyo ya soka itakutana Oktoba mosi, mwaka huu Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ambapo mashabiki wa Yanga wanadhani kuwa Chirwa atawakomesha.
Katika michezo ambayo Chirwa amecheza hajaonyesha uwezo mkubwa kama ilivyotarajiwa na kusababisha baadhi kumbeza, lakini mashabiki wa Yanga wanadhani kuwa nyota yake itaanza kuwaka kwa Simba.
 Katika mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita dhidi ya Mwadui FC, Chirwa hakupangwa na kuzua mjadala vijiweni kwamba anaandaliwa kwa ajili ya Simba hiyo Oktoba.
Rafael Mnandi, shabiki mkubwa wa Yanga, alisema kuwa wale wote wanaombeza Chirwa wanatakiwa kwenda uwanjani Oktoba wakaone jinsi anavyowaaibisha Simba.
 “Unaona hata mchezo dhidi ya Mwadui FC hakupangwa, yule anaandaliwa kwa ajili ya Simba, nawaambia kabisa atawaumbua siku hiyo,” alisema.
21 Sep 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top