May 6, 2025 04:09:21 AM Menu



KIKOSI cha Simba, leo kimefanya mauaji ya kutisha mbele ya Majimaji ya Songea baada ya kuichapa mabao 4-0 katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Simba ambayo inanolewa na Kocha Mcameroon, Joseph Omog na msaidizi wake Mganda, Jackson Mayanja, ilipata mabao yake kupitia kwa Jamal Mnyate aliyefunga mawili mengine yalifungwa na Shiza Kichuya, wachezaji hao wote wamejiunga na Simba msimu huu.
Kwa matokeo hayo, Simba imeendelea kukalia usukani kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 16 baada ya kushuka uwanjani mara sita ambapo imefanikiwa kushinda michezo mitano sare mmoja.
Huko Mtwara Azam FC imebanwa mbavu na kuacha alama tatu mbele ya Ndanda baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1.
  
24 Sep 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top