May 1, 2025 07:16:06 AM Menu



MFUMO wa Kocha wa Simba, Joseph Omog, unamfanya kiungo wa timu hiyo, Muzamir  Yassin, kushindwa kufunga mabao Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Muzamir aliyesajiliwa na Simba katika msimu huu akitokea Mtibwa Sugar, alikuwa na uwezo wa kufunga mabao kutokana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Meck Mexime, kuchezesha viungo watatu.
Muzamir alisema kwa sasa anashindwa kufunga katika kikosi cha Simba kutokana na Omog kutumia viungo wakabaji wawili.
Muzamir alisema Simba anacheza kama kiungo mkabaji na Jonas Mkude, huku Mwinyi Kazimoto na Said Ndemla viungo washambuliaji, kitu ambacho kinamfanya ashindwe kufunga mabao.
Muzamir alisema kutokana na mabadiliko ya mfumo wa uchezaji, anashindwa kupata nafasi ya kufunga mabao kama alivyokuwa Mtibwa Sugar.
“Nilipokuwa Mtibwa Sugar nilikuwa nafunga,  lakini hapa kinachoniangusha ni mfumo unaotumiwa na Omog ambao unanilazimu kukaba zaidi,” alisema Muzamir

15 Sep 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top