YANGA SC inatarajiwa kuondoka Ijumaa mjini Dar es Salaam
kwenda kisiwani Pemba kuweka kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wake wa
Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama ya Ghana Julai 16, Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga inahitaji ushindi wa kwanza katika mechi za kundi
hilo, baada ya kufungwa 1-0 mara mbili dhidi ya MO Bejaia nchini Algeria Juni
19 na TP Mazembe ya DRC mjini Dar es Salaam Juni 28, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Na Kocha Mkuu wa mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara, Hans van der Pluijm amesema kuhusiana na maandalizi yake
kuelekea mchezo dhidi ya Medeama anahitaji ushindi tu.
Akizungumza jana, Pluijm alisema kuwa matokeo ya ushindi
ambayo yatawapa pointi tatu muhimu ndiyo pekee wanayahitaji ili kufanya hesabu
wanazozitegemea kuwavusha na hatimaye kusonga mbele kwenye michuano.
Pluijm alisema bila kushinda mechi hiyo ya tatu, watakuwa
wamejiweka kwenye nafasi finyu ya kusonga mbele na hivyo ndoto za kuwania ubingwa
wa mashindano hayo yanayofanyika kila mwaka barani Afrika zitayeyuka.
"Soka ni mchezo wa makosa, sifikirii kama tutakosea
tena katika mechi hii ya tatu ya kundi letu, najua tutacheza tena nyumbani, ni
faida lakini kikuwa tunahitaji kushinda, tukifungwa...itakuwa ni majanga,"
alisema kocha huyo.
Mdachi huyo alisema watakapofanikiwa kushinda dhidi ya
Medeama, tayari nafasi kwa timu mbili zitakazosonga mbele kutoka kwenye kundi
hilo itakuwa wazi licha ya kupoteza michezo iliyotangulia.
Wakati huo huo kiungo mpya, Mzambia Obrey Chirwa ambaye
aliyekwenda kwao kwa ruhusa maaulumu, alirejea nchini jana kwa ajili ya
kuungana na wenzake kujiandaa na mechi hiyo dhidi ya Medeama.
TP Mazembe mabingwa mara tano wa Afrika kutoka Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ndiyo vinara wa Kundi A wakiwa na pointi sita
wakifuatiwa na Mo Bejaia yenye pointi nne, Medeama ina pointi moja na Yanga
ambayo haina pointi hata moja inaburuza mkia
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.