Na Faraja Yohana
Simba imemsajili Said Morad
aliyemaliza mkataba wa kuitumikia klabu ya Azam FC ili kuziba nafasi ya Hassan
Isihaka ambaye ameenda Mbao FC ya Mwanza mkopo.Morad amemaliza mkataba wake wa
mwaka mmoja aliopewa msimu uliopita lakini baada ya mkataba huo kumalizika
hajapewa mkataba mpya wa kuendela kubaki Chamazi.
Simba imemtoa Isihaka kwa mkopo
baada kushindwa kuendelea kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza cha
jeshi la Msimbazi.
Ikumbukwe nyota huyo
aliyechipukia kutoka kwenye timu ya vijana ya Simba, msimu uliopita
alihitilafiana na kocha wake Jackson Mayanja baada ya kugoma kucheza
kwenyechezo wa kombe la FA dhidi ya Singida United.
Post a Comment