April 11, 2025 11:57:03 AM Menu



Na Ariana Yohana
KIPA wa Barcelona, Marc-Andre ter Stegen amesema kuwa atabaki Nou Camp msimu ujao licha kuwa na tetesi za kutakiwa na klabu mbalimbali zikiwemo Manchester City na Liverpool za England.
Kipa huyo raia wa Ujerumani alizungumza hayo kwenye mtandao wa klabu na kusema ana furaha klabuni hapo na anataka kuendelea kubaki Barca.



Mtandao mwingine ulidai kuwa kipa huyo mwenye miaka 24, yupo tayari kuondoka kikosini hapo mwishoni mwa msimu huu na kujiunga na Pep Guardiola kwenye kikosi cha Man City.
Guardiola aliripotiwa kuwa anataka kuipiku Liver na kutoa pauni milioni 20 ili impate nyota huyo na huo utakuwa usajili wa kwanza mara baada ya kutua kikosini humo mwishoni mwa msimu huu.
Inadaiwa ter Stegen hafurahishwi na namna anavyopata nafasi kiduchu ya kucheza huku yeye akiwa kama back-up ya Claudio Bravo kwenye La Liga na nafasi kubwa ya kucheza anayo kwenye UEFA (wameshatolewa) na Copa del Rey.

05 May 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top