April 10, 2025 07:16:35 PM Menu



Na Ariana Yohana
KLABU ya Arsenal bado ipo kwenye mbio za kumuwania kiungo Granit Xhaka ambaye anamilikiwa na Borussia Monchengladbach kwenye majira ya joto.

Imeripotiwa kuwa Arsenal inafanya juu chini kuhakikisha inampata nyota huyo ili iweze kukiboresha kikosi chao tayari kwa msimu ujao.
Arsene Wenger anataka kurejesha matumaini kwa mashabiki wake ambao tayari wamemkatia tamaa kutokana na msimu huu kutoka kapa, kwa kufanya usajili mkubwa utakaowafanya watwae ubingwa wa EPL msimu ujao kutoka mikononi wa Leicester City.

Hata hivyo ripoti zingine zinasema kuwa pia klabu hiyo kutoka London inamuwinda pia nyota wa Borussia Dortmund, Henrikh ­Mkhitaryan, beki wa Atletico Madrid, Lucas Hernandez, nyota wa Leicester, Ben Chilwell na fowadi wa Inter Milan, Mauro Icardi.
                                                                                    


05 May 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top