April 12, 2025 03:24:27 AM Menu






DADA wa mchezaji Patrick Ekeng, ambaye alifariki baada ya kudondoka uwanjani katika mchezo kati ya Dinamo Bucharest na Viitorul Constanta Ijumaa usiku, amesema Ekeng alikuwa anajihisi kuchoka kupita kiasi kabla ya mechi hiyo.

Ekeng, 26, raia wa Cameroon alianguka na kufariki dakika ya 69 ikiwa ni dakika saba tu tangu aingie akitokea benchi. Inaelezwa kuwa alipata shambulio la ghafla la moyo.
“Alimwambia rafiki yake mkubwa kuwa hayupo tayari kucheza mechi hiyo,” alisema Monique Chantal, ambaye ni dada mkubwa wa Ekeng. "Alisema amechoka sana."
Dada huyo aliongeza: "Patrick ni mtu anayejiamini na kujituma muda wote. Ni maumivu makubwa kwani ameondoka na ameiachia machungu familia, ni kama ndoto mbaya ya usiku."
Mama yake Ekeng, Celine Chemi alisema: "Ni vigumu kuzungumzia kifo cha mtoto wangu, lakini ninaamini hii ni mipango ya Mungu.”
Kuna habari kwamba, Ekeng hakupatiwa huduma ya kwanza inayostahili kitu kilichosababisha kifo chake. Hata hivyo, daktari wa Dinamo Bucharest, Liviu Batineanu alisema: "Mchezaji alianguka, tukamuwahi haraka bila ruhusa ya mwamuzi, tulijitahidi kuokoa uhai wake.”
09 May 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top