April 10, 2025 06:57:50 PM Menu






KWA mujibu wa magazeti ya Uturuki, inadaiwa kuwa Klabu ya Fenerbahce ipo mstari wa kwanza kumuwania staa wa Valencia, Sofiane Feghouli ambaye anatarajiwa kuondoka baada ya kumaliza mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Ukiachana na Waturuki hao kumtaka nyota huyo, lakini pia klabu kutoka England, United, Liverpool and Tottenham zimeripotiwa kuwa zina mvizia nyota huyo ili zimsajili.


Inadaiwa kuwa Feghouli ambaye ni raia wa Algeria amekuwa hayupo kwenye wakati mzuri kikosini humo na mwezi uliopita alisimamishwa baada ya kuripotiwa kuwa aligoma kufanya mazoezi na timu.
Kiungo huyo mchezeshaji mpaka sasa amecheza mechi 21 za La Liga na amefunga bao moja huku akitoa asisti mbili.
"Sijui kama Sofiane Feghouli ataivaa tena jezi ya Valencia,” alisema Kocha wa Valencia, Pako Ayestaran. Feghouli alijiunga na kikosi hicho Mei 2010.

04 May 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top