April 11, 2025 07:59:17 AM Menu




BAADA ya uongozi wa Simba kuridhishwa na kazi kubwa iliyofanywa na beki wa kulia raia wa DR Congo, Janvier Bokungu katika mzunguko wa kwanza, unatarajia kumuongezea mkataba mwingine wa miezi sita utakaofikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

Bokungu ambaye alijiunga na Simba hivi karibuni, mkataba wake wa awali ulikuwa unafikia tamati Januari, mwakani.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Bokungu alisema kuwa tayari ameshafanya mazungumzo na uongozi wa Simba na anachosubiri tu ni kusaini mkataba huo.
“Wao walitaka wanipatie mwaka mmoja lakini nikawaomba wanipatie miezi sita ili niweze kumalizia msimu huu, baada ya hapo ndipo tutakaa na tuzungumze kuhusiana na mkataba wa muda mrefu.
“Hata hivyo, kama Mungu akipenda basi kesho (leo) ninaweza kusaini mkataba huo na baada ya hapo ndipo nitaondoka zangu kwenda nyumbani kwa mapumziko,” alisema Bokungu.

21 Nov 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top