LICHA ya kwamba Yanga leo Jumatatu inaanza rasmi
kambi yake ya kujiwinda na mzunguko wa pili wa ligi, beki wa kikosi hicho,
Mtogo, Vincent Bossou, hatakuwepo katika kambi hiyo kutokana na kuelekea nchini
Vietnam.
Bossou ambaye anaunda safu ngumu ya ulinzi ya
timu hiyo akishirikiana kwa ukaribu na Kelvin Yondani na Andrew Vicent ‘Dante’,
wameweza kuisaidia timu hiyo kumaliza katika nafasi ya pili katika msimamo wa
ligi ikiwa na pointi 33 nyuma ya Simba yenye 35.
Leo Yanga inaanza mazoezi kwa mara ya kwanza
ikiwa chini ya kocha Mzambia, George Lwandamina baada ya Mholanzi, Hans van Der
Pluijm kubadilishiwa majukumu, akipelekwa kuwa Mkurugenzi wa Ufundi klabuni
hapo.
Hata hivyo, Bossou hatakuwepo katika mazoezi hayo
chini ya Lwandamina.
Bossou ameweka bayana kwamba atachelewa kujiunga
na wenzake Jumatatu kutokana na kumpeleka ndugu yake nchini Vietnam kusaini
mkataba na moja ya timu za nchini humo ambapo atatua hapa nchini Desemba 3.
“Mimi nitarudi nchini Desemba 3, siku sita baada
ya kambi kwa ajili ya kujiunga na wenzangu pamoja na kocha mpya George
Lwandamina, nitakosekana kwa siku hizo kwa sababu nitasafiri kuelekea nchini
Vietnam.
“Naenda kumsindikiza ndugu yangu kusaini mkataba
na moja ya timu za huko pamoja na mimi mwenyewe kumalizana na timu ambayo
nitaenda kujiunga nayo baada ya mkataba wangu kumalizika hapa Yanga,” alisema
Bossou anayetarajiwa kumaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu.
Related Posts
- Tumewasikia, tunawathamini, tunawapenda, tutarejea14 May 20170
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...Read more »
- Caf kuilipia Yanga mishahara25 Dec 20160
YANGA inahesabu siku tu kabla ya kuanza kuogelea mamilioni ya fedha za Shirikisho la Soka barani...Read more »
- Tatizo la Okwi kwishnei Simba25 Dec 20160
BADO mashabiki wa Simba wanaendelea kumkumbuka straika wao Mganda, Emmanuel Okwi, kutokana na ka...Read more »
- Kocha wa Wacomoro atamba kuibania Yanga Caf24 Dec 20161
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...Read more »
- Wakala: Ajibu hawezi kucheza popote, anawatikisa Simba tu24 Dec 20160
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...Read more »
- SIMBA WANACHEEEEEEEEEEEEKAAAAAAAAAAAAA24 Dec 20160
SARE ya bao 1-1 waliyoipata Yanga jana dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru, imezidi ku...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.