April 11, 2025 08:59:02 AM Menu



KOCHA Mkuu wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog, amesema kuwa anafurahishwa na kasi kubwa ya kikosi chake kwenye michuano ya Ligi Kuu Bara msimu huu, hali inayomfanya aamini kuwa watatangaza ubingwa mapema.

Simba ndiyo inayoongoza msimamo wa ligi kuu, ikiwa na alama 35 huku wanaowafuatia ambao ni Yanga wakiwa na 30.

Omog alisema kuwa anataka timu yake hiyo itangaze ubingwa mapema ili pia iweze kupata muda mzuri wa kuwania Kombe la FA.
Kauli hiyo ya Omog ni kama ya uchokozi kwa Yanga kwani inaonekana kulenga kutaka kuipokonya timu hiyo makombe hayo yote iliyoyapata msimu uliopita.
 “Namshukuru Mungu kwa mwenendo huu wa timu yangu ambao imekuwa ikienda nao katika harakati zetu za kuwania ubingwa wa ligi kuu.
“Hata hivyo, nataka katika mzunguko wa pili, kasi hii iongezeke ili tuweze kutangaza ubingwa mapema kabisa ili tupate muda mwingine wa kujiandaa na michuano ya Kombe la FA ambalo nalo tunataka tulichukue,” alisema Omog.
07 Nov 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top