April 10, 2025 01:13:54 AM Menu




UONGOZI wa Klabu ya Yanga umekubaliana na Kocha Hans van Der Pluijm kuchukua nafasi ya Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo.

Awali, Pluijm alikuwa anachukua nafasi ya Mkurugenzi wa Ufundi ambayo kawaida angekuwa chini ya Kocha George Lwandamina lakini sasa Pluijm anakuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Yanga, maana yake ni bosi juu ya Lwandamina.

Taarifa za ndani zimeeleza Yanga wamefikia mwafaka na kocha huyo kuhusiana na cheo hicho na mwenyewe pia anaonekana kukubali.

“Kweli kila kitu kimeenda vizuri kati ya Yanga na kocha. Walikaa vikao viwili na mambo yameenda vizuri kabisa.

“Kikubwa ilikuwa ni kujua kocha atafanya nini, maana Yanga nao pia walikuwa wakitaka kila kitu kiwe safi.”

Alipotafutwa jana Pluijm, alijibu: “Kweli bado niko Dar, subiri nitakupigia baada ya kikao.”

Hata hivyo hakupiga, ilipofika jioni alipotafutwa tena, simu yake iliita bila ya kupokelewa na alipopigiwa tena, akakata na kuizima, twiiii.

Yanga imekuwa ikipambana kumbakiza kocha huyo licha ya kumchukua Lwandamina ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili kuinoa.
CHANZO: CHAMPIONI
18 Nov 2016

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top