Shirikisho la Soka Barani Afrika, CAF kupitia kwa bodi yake
ya masuala ya nidhamu imeipiga klabu ya Yanga faini ya dola za kimarekani 10,
000 sawa na zaidi ya milioni za shilingi za Tanzania.
Faini hio ya CAF imetolewa kutokana wachezaji wa Yanga
kupinga maamuzi ya mwamuzi katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa Kombe la
Shirikisho dhidi ya Esperanca Sagrada ya Angola.
Hata hivyo, Yanga
imepewa nafuu ya kulipa nusu ya kiasi hicho na kutakiwa kulipa kiasi kingine
endapo tu itarudia kosa hilo.
katika mchezo, Sagrada walipewa penati dakika ya mwisho ya
pambano pamoja na nahodha wa Yanga kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Hata hivyo Yanga ilifanikiwa kufuzu kwa hatua ya makundi
baada ya kufungwa bao 1-0 na hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao
2-1.
Post a Comment