KAMA kuna mtu mwenye furaha kwa sasa kutokana na kupata kazi mahali alipokuwa akifukuzia kwa muda mrefu basi ni Jose Mourinho.
Na kuhitimisha furaha yake hata mjengo wake anaotaka kwenda kuishi ndani ya Jiji la Manchester basi ni mkali kwelikweli.
Kuna mjengo wa maana wenye thamani ya Pauni 5 milioni, ambao una vyumba pia chini ya ardhi, umewekwa kwenye orodha ya makazi anayotaka kwenda kuishi kocha huyo raia wa Ureno.
Jumba hilo halipo kwenye kijiji maarufu cha wanasoka huko Cheshire, lakini taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo imefichua kwamba makazi hayo ni mwafaka na yanafaa kabisa kwa Mourinho na familia yake.

Taarifa za ndani zimefichua kwamba Mourinho amekuwa akitafuta nyumba ya kifahari kwa wiki sita sasa na yeye pamoja na watu wake walikwenda kulitazama jumba hilo la Steppingstones mara mbili tofauti.
Jumba hilo lipo Frodsham, Cheshire, linamilikiwa na mmiliki wa klabu ya ligi ya rugby, Widnes Vikings, Steve O’Connor limetajwa kuwa bei yake ni Pauni 4.75 milioni.
Kwenye eneo hilo la jumba analotaka kununua Mourinho baada ya sasa kuwa kocha wa Manchester United, kuna nyumba pia ilinunuliwa na staa wa zamani wa Liverpool, Djibril Cisse mwaka 2005.
Chanzo kutoka ndani ya klabu ya Man United kilieleza: “Si jambo la kificho kwamba watu wa Mourinho wamekuwa wakitafuta nyumba yenye nafasi katika eneo hilo inayofaa kuishi yeye na familia yake.

“Nyumba hiyo inauzwa na tumesikia kwamba Mourinho na mkewe walikwenda kwa siri kutazama eneo hilo. Walikwenda kwenye nyumba nyingine pia.
“Ni mahali pazuri na kuna mazingira yanayowafaa kabisa. Ni umbali wa nusu saa tu kufika kwenye uwanja wa mazoezi.”
Milionea Steve O’Connor alihamia kwenye nyumba hiyo mwaka 2010. Jumba hilo lina uwanja wa helikopta, bwawa la kuogelea, uwanja mdogo wa soka, baa na sehemu ya kupumzikia ya nje yenye televisheni kubwa kabisa.
Jumba lenye teknolojia ya kutosha kabisa, milango inayofunga na kufungwa bila ya kutumia ufunguo, milango ya kufungua kwa alama za vidole sehemu ya kumpumzika juu ya paa.

O’Connor alisema: “Huwezi kuipata nyumba kama hii mahali popote pale. Ni nyumba yenye teknolojia mchanganyika za karne ya 16 na 17 na teknolojia za kisasa.”

Post a Comment

 
Top