UJIO wa kiungo mkabaji Mzambia, Justine Zullu 'Mkata Umeme' huenda ukawa na mafanikio kwa winga, Simon Msuva kutokana na aina yao ya uchezaji ilivyo, kwani wameonyesha kuelewana.
Kiungo huyo mwenye sifa kubwa ya kukaa na mpira na kupiga pasi zenye macho, alitua nchini wiki moja iliyopita kutoka kwao Zambia kwa ajili ya kuichezea timu hiyo inayojiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Zullu amefanya mazoezi ya pamoja na timu hiyo kwa siku sita kwenye Viwanja vya Gymkhana, Posta jijini Dar es Salaam na kuonyesha uwezo mkubwa hasa katika kukaba na kupiga pasi zenye macho.
Katika mazoezi ya timu hiyo ya kimbinu waliyoanza kuyafanya wiki hii, kiungo huyo mwenye umbile kubwa, mara zote amekuwa akipangwa kucheza pamoja na Msuva.
Zullu alionekana akicheza kwa kuelewana na Msuva kwa kumpigia pasi ndefu pembeni na kufika miguuni mwa winga huyo, ambaye alimiliki mpira na kuanza kufukuzana na mabeki au kupiga krosi safi.
Msuva alionekana kunogewa na pasi hizo ndefu ambazo awali zilikuwa zikipigwa na kiungo, Athumani Idd 'Chuji' na kuonekana uwanjani muda wote akijitenga pembeni akiwatoroka mabeki akisubiria pasi hizo.
Wachezaji hao, kuna wakati walikuwa wakisogeleana wakipigiana pasi fupi wakiwa wanalishambulia goli la wapinzani wao na Msuva kufanikiwa kutengeneza bao lililotokana na krosi safi aliyoipiga baada ya kupokea pasi ya Zullu. Bao hilo lilifungwa na Donald Ngoma.
Akimzungumzia Zullu, Msuva alisema: “Ni mchezaji mzuri mwenye uwezo wa kumiliki mpira na kupiga pasi, ninaamini kama tukikaa pamoja tukicheza kwa kuzoeana, tutafanya vitu vingi vizuri.”
Related Posts
- Tumewasikia, tunawathamini, tunawapenda, tutarejea14 May 20170
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...Read more »
- Caf kuilipia Yanga mishahara25 Dec 20160
YANGA inahesabu siku tu kabla ya kuanza kuogelea mamilioni ya fedha za Shirikisho la Soka barani...Read more »
- Tatizo la Okwi kwishnei Simba25 Dec 20160
BADO mashabiki wa Simba wanaendelea kumkumbuka straika wao Mganda, Emmanuel Okwi, kutokana na ka...Read more »
- Kocha wa Wacomoro atamba kuibania Yanga Caf24 Dec 20161
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...Read more »
- Wakala: Ajibu hawezi kucheza popote, anawatikisa Simba tu24 Dec 20160
Normal 0 false false false EN-US X-NONE X-NONE ...Read more »
- SIMBA WANACHEEEEEEEEEEEEKAAAAAAAAAAAAA24 Dec 20160
SARE ya bao 1-1 waliyoipata Yanga jana dhidi ya African Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru, imezidi ku...Read more »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.