WACHEZAJI soka wanaume wanapokuwa
wameweka ukuta wakati wa faulo huwa ni kawaida yao kuweka mikono mbele katikati
ya miguu yao ikiwa ni sababu maalum kutokana na maumbile yao, sasa mwanasoka wa
kike naye amefanya hivyo na kuwashangaza wengi.
Nothando Vilakazi ni mchezaji wa timu
ya soka ya wanawake ya Afrika Kusini iliyokuwa ikishiriki katika Michezo ya
Olimpiki, alinaswa na kamera akiweka mikono hiyo kama wanaume wanavyofanya
wakati wa mechi dhidi ya Brazil.
Vilakazi aliweka mikono hiyo huku
wenzake wakiwa hawajaweka jambo ambalo lilisababisha picha yake isambazwe kwa
wingi mitandaoni wakihoji sababu za yeye pekee kufanya hivyo.
Post a Comment