KOCHA wa Mo Bejaia ambayo jana ilicheza na Yanga na kupokea kichapo cha bao 1-0, Nacer Sandjak ameibuka na kusema Obrey Chirwa na mlinzi Vicent Bossou ndiyo walikuwa shida kwao kupata ushindi.

Akizungumza na spotiripota.blogspot.com,  Nacer Sandjak alisema mchezaji wa Yanga aliyevaa jezi namba saba ambaye ni Chirwa ndiye alikuwa nyota wa mchezo kwa upande wa washambuliaji huku upande wsa ulinzi akitaja beki aliyevaa jezi namba tisa ambaye ni Bossou.


"Mchezaji aliyevaa namba 7 ndiye aliweza kuisumbua sana ngome yangu ya ulinzi pia safu ya ulinzi ni yule aliyevaa jezi namba 9. Yanga wamebadilika sana kuliko tulivyocheza nao nyumbani . Wamekuwa na nidhamu nzuri katika ukabaji na kutengeneza presha ya mashambulizi langoni kwetu ."

Post a Comment

 
Top